Watumishi wa PSSSF kundi la wakimbiaji (PSSSF RUNNERS), wametoa misaada mbalimbali ya kijamii kwa Kituo cha Watoto Yatima cha Kisarawe (Kisarawe Orphanage Center), mkoani Pwani, ikiwa ni sehemu ya kuonesha ushirikiano na upendo kwa jamii.
Akikabidhi misaada hiyo, kiongozi wa kundi hilo, Mohamed Iddi Nyallo, amesema hatua hiyo ni kuthibitisha kauli mbiu ya PSSSF ya 'Leo. Kesho Pamoja'. Amesema, misaada iliyotolewa ni mahitaji mbalimbali, ikiwemo vyakula, vifaa vya kuhifadhia maji na vifaa vya shule.
"Misaada hii imetokana na michango ya hiayari kutoka kundi la Watumishi wakimbiaji wa PSSSF (PSSSF RUNNERS)." Amefafanua Nyallo.
Amesema "Sisi kama watumishi wa Mfuko tuliona badala ya kukutana sisi wenyewe na kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya, tulikubaliana tukusanye fedha ili tununue mahitaji ya kusaidia vituo vya kulea watoto wenye uhitaji; Tumepanga kusaidia vituo vitatu na tumeanza na hiki cha Kisarawe." Amesema.