Serikali imekusudia kujenga bandari ya Kisiwa - Mgao Mkoani Mtwara ambayo itatumika kusafirisha bidhaa chafu kama vile Mbolea, Saruji na Makaa ya Mawe.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa amebainisha hayo Desemba 19, 2024, alipozungumza na Waandishi wa habari baada ya kutembelea na kukagua eneo unapotekelezwa mradi huo unaotarajiwa kuanza kutekelezwa tarehe 03/01/2025 na kukamilika tarehe 03/07/2027.
Ujenzi wa bandari hiyo unafanywa na Mkandarasi kutoka Nchini China M/S China Harbour Engineering Company Limited (CHEC) kwa gharama ya shilingi bilioni 434.5 ambazo ni fedha za ndani za Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania.
Ameeleza kuwa hatua hiyo itawezesha shughuli za usafirishaji makaa ya mawe katika Bandari ya Mtwara kuhamia katika eneo hilo, hivyo kuondoa changamamoto ya vumbi na kuongeza ufanisi katika shughuli za usafirishaji.