NB:PICHA NA MAKTABA
Matengenezo ya mitambo mitatu ya kufua umeme yasababisha baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam kukosa umeme kwa muda.
Shirika la umeme nchini (TANESCO) limesema kukosekana kwa huduma ya umeme katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam kunatokana ukarabati wa mitambo mitatu ya kufua umeme kwa kutumia gesi asili katika kituo cha Ubungo namba mbili na si mgao wa umeme.
Akizungumza wakati wa ziara ya Katibu mkuu wa wizara ya nishati katika kituo cha kufua umeme cha Ubungo, Meneja wa kituo cha Ubungo namba mbili mhandisi Lucas Busunge amesema matengenezo wa mtambo huo yalipangwa kukamilika mwezi Februari mwaka huu lakini kutokana na ukaguzi wa mtambo kubaini baadhi ya vipuri vimeharibika mkandarasi ameamua kuagiza vipuri nchni Sweden na kufanya muda wa matengezo kuongezeka hadi Machi moja mwaka huu.