![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/tafaa.jpg?itok=nH3hOF6V)
Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine ulimwenguni kuanzimisha Siku ya mtoto wa Afrika Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ametuma ujumbe maalum kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kwa kuwataka watafakari ni kwa kiwango gani wanatetea na kulinda haki za mtoto na kivipi wanatimiza wajibu wa kuwapa malezi bora na furaha.
Mwaka huu kaulimbiu ya Siku ya Mtoto wa Afrika inasema, "Tutekeleze ajenda 2040: kwa Afrika inayolinda haki za mtoto".