Back to top

Ndege za Urusi zapigwa marufuku anga la Umoja wa Ulaya

27 February 2022
Share

Umoja wa Ulaya umetangaza kufunga anga lake kwa ndege zote zinazomilikiwa, zilizosajiliwa na zinazodhibitiwa na Urusi ambapo Rais wa Umoja huo Ursula von der Leyen amebainisha kuwa ndege hizo hazitaweza kutua, kupaa au kuruka juu ya eneo la Umoja wa Ulaya huku akisisitiza kuwa marufuku hiyo inajumuisha ndege za kibinafsi za oligarchs.