Back to top

Changamoto za kiufundi, ATCL kupunguza safari

10 November 2022
Share

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limetangaza kuwa litapunguza miruko na kufuta baadhi ya safari zake kutokana na changamoto za kiufundi kote duniani za injini aina ya PW1524G-3 zinazotumika katika ndege za Airbus A220-300, ambapo limebainisha kuwa katika kuzingatia matakwa ya kiusalama, shirika hilo limekuwa likifuata maelekezo ya kitaalam ili kutoa huduma bora na ya usalama hivyo, wakati mwingine limekuwa likizitoa ndege hizo kwenye mzunguko, kukidhi matakwa ya watengenezaji wa injini hizo.