![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/NIDA%20SITE.jpg?itok=wP9qAYzh)
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Geofrey Tengeneza, amesema Mamlaka hiyo imezindua mfumo wa kusajili watu kwa njia ya mtandao, ili kuwawezesha wananchi wenye sifa, kuomba vitambulisho hivyo bila kwenda kwenye ofisi za usajili za Wilaya au vituo vya usajili vya mamlaka hiyo.
.
Hata hivyo, mfumo huo hautawahusu wale ambao tayari wana vitambulisho na wanahitaji kuvihuisha ifikapo Januari 2023, kwani watalazimika kwenda moja kwa moja ofisi za NIDA kwa ajili ya kuingiza baadhi ya taarifa mpya na kupiga picha.