Back to top

IDADI MIILI WALIOFUNGA HADI KUFA KENYA, YAFIKIA 83

25 April 2023
Share

Idadi ya miili ya waumini wa kanisa la Good News International wanaoaminika kufunga hadi kufa, baada ya kuamriwa kufanya hivyo na Mchungaji wao Bw.Paul Makenzie, iliyofukuliwa katika eneo la Shakahola, nchini Kenya, imefikia 83, baada ya miili mingine 10 kufukuliwa mapema leo jumanne, Aprili 25, 2023.
.
Waziri wa usalama nchini humo, Kithure Kindiki anatarajiwa kutembelea msitu huo leo, huku Mamlaka za usalama zikiwa na wasiwasi kuwa huenda idadi ya miili ikaongezeka.