Back to top

PIKIPIKI YAUA MUME NA MKE MTWARA.

18 December 2023
Share

Watu wawili ambao ni mtu na mke wake wamefariki dunia  baada ya pikipiki waliyopanda kuacha njia na kugonga gema katika Mlima Kinombedo uliyopo kijiji cha Mkwiti wilaya ya Newala mkoa Mtwara majira ya saa moja asubuhi.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara  Nicodemus Katembo inasema  pikipiki iliyopata ajali ni aina SUN LG yenye namba za usajili MC 828 BUT huku chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kumudu pikipiki hiyo.

Kamanda Katembo amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Ismail Hajili Chitapwidi,  na mkewe ni Aisha Bakari Chilambo ambapo ametoa rai kwa watumiaji wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani, na kuwasihi abiria kuvaa kofia ngumu.