Back to top

10 WAFARIKI DUNIA, AJALI YA LORI LA POLISI NA KIRIKUU, SIHA

18 August 2023
Share

Watu 10 wamefariki dunia na mwingine mmoja kujeruhiwa baada ya Lori la Polisi kugongana na gari dogo la mizigo (KIRIKUU), katika eneo la Datch Conner, Siha mkoani Kilimanjaro.
.
Mkuu wa Wilaya ya Siha Christopher Timbuka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, huku akibainisha kuwa katika ajali hiyo waliofariki wanawake ni 6 na Wanaume 4, majeruhi wapo katika hospitali ya Siha na Maiti imehifadhiwa hospitali ya Kibon'oto, ambapo taratibu za kutambua waliofariki zinafanyika.
.
Timbuka amesema chanzo cha ajali hiyo ni kuyumba kwa Kirikuu, baada ya kupata shida kwenye gurudumu la kulia na kusababisha kugongana uso kwa uso na lori la Polisi.