Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Imemkamata afisa wa mamlaka ya mapato nchini TRA mkoa wa Ilala bw. Elias Athuman Yunus kwa tuhuma za kuomba rushwa ya dola elfu 17.
Kaimu mkuu wa takukuru Ilala bw. Enos Ngailo amesema mtuhumiwa aliomba rushwa kwa mkurugenzi wa kampuni ya HEM- HEVY Equipment Company ltd ili kutoa taarifa za uongo kuhusu usajili wa mitambo iliyoingizwa nchini kwa lengo la kukwepa kodi.
Amesema uchunguzi wa TAKUKURU umebaini mtuhumiwa aliomba milioni 50 na baada ya majadiliano alipunguza hadi milioni 35 ambazo alitaka zilipwe kwa mfumo wa dola za marekani.
Bw. Ngailo samesema mtuhumiwa alikamatwa baada ya kupokea dola elfu moja.