Back to top

BUCHOSA: MABALOZI WALIA MAJINA YA WAJUMBE KUONDOLEWA

07 April 2025
Share

Mabalozi wa mashina  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza hususani Jimbo la Buchosa, wamelalamikia baadhi ya viongozi wa Matawi na Kata kuenguliwa majina ya wajumbe na kuwekewa wajumbe wasiowafahamu kinyume na matakwa ya Chama Cha Mapinduzi.


Miongoni mwa viomgozi wanaolalamikiwa na Mabalozi hao ni Mwenyekiti wa  (CCM) Kata ya Kasisa jimboni Buchosa, Bw. Maxamilian Rulanga  ambaye aliwaita baadhi ya mabalozi wa kata ya hiyo kwa lengo la kuwashinikiza wabadili majina wa wapiga kura ili wamchague mtia nia anayemtaka. 

Jambo hilo lilipingwa vikali nabadhi ya mabalozi wakidai hawawezi kufanya hivyo  bora wapoteze uhai lakini haki itendeke siyo kuwachagulia wapiga kura wao.

Mabalozi hao wamezitaka mamlaka  husika kuchukua hatua dhidi ya viongozi ambao wanakwenda kinyumbe na kanuni za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wiki moja baadae mmoja wa mabalozi waliohudhuria kikao hicho  Michael Tuluchengwa alifariki dunia, huku  kifo chake kikiwa cha  kutatanisha kwa  madai kuwa alinyweshwa sumu kwenye pombe. 

Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo aliongoza wananchi wa Buchosa kwenye maziko hayo  ambayo wanachi wa Buchosa walisikitishwa na kifo hucho.

Juhudi za Mwenyekiti huyo ambaye aliambatana na katibu kata wake Reonce Baseza ziligonga mwamba baada ya mabalozi hao kumgomea kubadili  majina  wakidai wapo tayari kufa lakini  haki itendeke kwa Mbunge wao wa Jimbo hilo la Buchosa  Eric Shigongo ambaye amefanya kazi kubwa jimboni humo na anakubalika na wananchi. 


“Mwenyekiti kama ni kufa mimi nipo tayari niwe wa kwanza kufa lakini haki itendeke…” alisikika akisema Balozi  Matatizo Mlola  kutoka shina namba 35 tawi la Kasisa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kasisa Maxamilian Rulanga amesema kikoa hicho waliitwa baadhi ya mabalozi wa tawi la Kasasi lengo lilikuwa ni kuwapatia taarifa kuwa majina ya wajumbe wa mabalozi yalikwishapelekwa wilayani toka mwaka 2022 hivyo wasiteuwe wengine ndipo ilipoibuka sintofahumu hiyo na kikao hicho kilikuwa nichamaelekezo pekee.


Tangu CCM ibadili katiba na kuongeza idadi ya wapiga kura, umeibuka mchezo jimboni Buchosa wa kutaka kubadili majina ya wapiga kura waliiongezeka ili kumsaidia mtia nia mmoja ambaye inaonekana kwa njia halali hawezi kushinda. 


Haya yakitokea ofisi ya CCM wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wake Marco  makoye imekuwa kimya jambo linalotafsiriwa kama vurugu hizi pengine zina baraka ya Ofisi ya (CCM)  wilaya ya Sengerema.


Hivi karibuni Waridi Mngumi, aliyekuwa Katibu wa Wilaya ya Sengerema yenye majimbo ya Buchosa na Sengerema aliahamishwa ghafla kutokana na kinachodaiwa kuwa ni kufumbia macho fujo zinazoendelea Buchosa. 


Siku chache zilizopita Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Bw. Omari Mtuwa, aliitisha mkutano mkuu wa jimbo na kukemea vikali fujo zinazoendelea Buchosa na kwamba hatasita kumchukulia hatua kali mtu yeyote ambaye ataendeleza fujo hizo. 


Katika hali ya kushangaza siku mbili baada ya mkutano huo Mwenyekiti wa (CCM) Kata ya Kasisa Maxamilian Rulanga aliwaita baadi ya mabalozi na kuwapa vitisho lakini wamegoma na  kuendelea na   msimamo wao wa kugoma kubadili majina.

Balozi wa Matatizo Mlola shida 35 tawi la Kasasi amesema yuko tayari kupoteza uhai wake lakini apiganie haki ya wazee wake balozi walejeshwe na siyo kupangiwa na katibu tawi na katibu kata wa Kata ya Kasisa.