
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa amesema serikali ipo katika hatua muhimu za kuanza ujenzi wa reli ya kisasa ya treni za mwendokasi (SGR) katika mikoa ya kusini.
Akizungumza wakati wa kikao kazi cha menejimenti ya TRC na waandishi wa habari mkoani Morogoro, Bw. Kadogosa amesema tayari taasisi za kifedha zimeonesha nia ya kutoa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 2.4 (zaidi ya Sh trilioni 6.4) kufanikisha ujenzi huo.
"Kuna uwezekano tukaanza ujenzi wa reli ya kusini, tumedhamiria kuanza ujenzi huu na mpango mwingine ni ule unaohusisha ujenzi wa reli ya kilometa 1,053 kutoka Tanga hadi Musoma kupitia Arusha"
Aidha, Bw. Kadogosa amesema maeneo hayo pia yanafursa hasa usafirishaji wa mizigo kutokana na shughuli za kiuchumi zikiwemo uchimbaji wa madini.