Back to top

WANANCHI WATAKIWA KUISHI MAISHA YA KUMPENDEZA MUNGU

27 March 2025
Share

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula amewaasa Wananchi kuishi maisha ya kumpendeza mwenyezi Mungu Katika kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani wakiwa na amani, upendo na usalama.


Amezungumza hayo wakati akimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas  Ndumbaro Katika tukilo la kufuturisha lililofanyika kwenye ofisi ya Katiba na Sheria  jijini Dodoma.

Amesema kuwa, lengo la kufuturisha ni kujumuisha wadau wote wa Katiba na Sheria  wakiwemo viongozi wa Dini ya Kiislam katika kuenzi maandiko matukufu ya Mungu.

"Wizara ya Katiba na Sheria ni Wizara inayosimamia Haki. Katika kipindi hiki cha Ramadhani Wananchi wanapaswa  kuishi kwa upendo wakimpendeza Mwenyezi Mungu, ikiwa wanazingatia Amani na Usalama wa Nchi" amesema

" Leo Wizara imeandaa Futari kwa ajili ya Watumishi  pia tuliwaalika  Watumishi wa Mungu akiwemo  Shekhe Mkuu wa  Mkoa pamoja na jopo lake lengo ilikuwa ni kukutana na kujumuika kwa pamoja katika kupata futali ya pamoja na kusikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu" amesema


Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustaph Rajabu ameisii jamii iwe na utamaduni wa kushukuru pamoja na kufanya Ibada huku akieleza kuwa mtu mwenye kufuturisha anapata thawabu  sawa na mtu aliyefunga.


"Mtu mwenye kufturisha atakuwa na malipo kama yule mfungaji aliyefunga na yoyote anayealikwa kwenye karamu aende asipoenda anapata dhambi."

Aliendelea kusema " atakayekutendeeni jambo jema mlipeni kwa wema  na kama ukupata cha kufanya basi muombee Mungu, asiyeweza kushukuru kidogo kwa binadamu mwezie aliyemtendea wema ata akipewa mlima wa dhahabu awezi kushukuru." alimalizia

Naye Shekhe Mohamed Saidi amesema kuwa katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani Wananchi waombe kwa ajili ya Nchi pamoja na  Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu ili uwe Uchanguzi wa Amani, Salama na Haki 

"Katika kipindi hiki cha Ramadhani kuna kila sababu ya kuombea Nchi yetu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchanguzi Mkuu wa Mwaka  2025 , tunachoomba Mwaka huu ni kufanya Uchanguzi kwa Salama na  Amani." Alihitimisha