Back to top

Agizo la Serikali latekelezwa kwa vitendo Ushetu Kahama.

17 July 2018
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama kutekeleza kwa vitendo agizo la rais John Pombe Magufuli la kuhakikisha wataalamu wa kilimo na maofisa Ugani wanatoka maofisini na kuwafuata wakulima Mashambani.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akizindua na kukabidhi pikipiki na gari mpya aina ya ToyotaLlandcruiser Hard-Top lililonunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani ya halmashauri hiyo ili litumiwe na maofisa wa kilimo kufuatilia shughuli za kilimo kwa wakulima ambapo ameitaja halmashauri ya Ushetu kuwa ni ya mfano wa kuigwa na halmashauri zingine nchini.

Akizungumza kabla ya waziri mkuu kuzindua na kukabidi pikipiki 21 zilizonunuliwa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya,pikipiki 3 na gari hilo kwa ajili ya idara ya kilimo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tekack ametaja gharama zilizotumika kununua vifaa hivyo.

Kufuatia hali hiyo waziri wa kilimo Mhe. Charles Tizeba ameahidi kuipatia halmashauri hiyo trekta 2 za kisasa kwa lengo la kuwasaidia wakulima kuondokana na kilimo cha jembe la mkono na ya kukokotwa kwa Ng'ombe hali inayotarajiwa kuongeza mavuno ya mazao ya biashara na chakula.