
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi.Sophia Mjema, kufuatia vifo vya watu 16 , vilivyotokea katika ajali ya gari Agosti 08, 2022 , katika Kata ya Mwakata, wilayani Kahama.
.
Aidha Rais Samia amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia usalama barabarani kuongeza juhudi za kudhibiti ajali.