
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 5 na majeruhi 10 kufuatia ajali iliyohusisha Daladala na Lori katika eneo la Chang'ombe Temeke Dar es Salaam.

Kati ya hao majeruhi 10 wa nne hali zao ni mbaya na wamepelekwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Amesema ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva wa daladala,"Dereva wa Daladala alifanya uzembe mkubwa, kwa kupita kwenye mataa wakati taa nyekundu inawaka"-Mambosasa.
Jeshi hilo limesema huo ni uchunguzi wa awali, hivyo wanaendelea na uchunguzi.