Back to top

Akamatwa akisafirisha kg.390.75 za mirungi

11 September 2022
Share

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limemkamata Allen Wilbard Kasamu, miaka 49, Dereva na Mkazi wa Suye-Moshono Jijini Arusha akiwa anasafirisha madawa ya kulevya aina ya mirungi yenye uzito wa kg.390.75 kwa kutumia gari la kubebea mafuta aina ya Mitsubish Canter - Tanker ambapo Jeshi hilo limesema kuwa Mtuhumiwa huyo alitumia mbinu ya kupakia madawa hayo ndani ya tenki la mafuta.