Serikali mkoani Geita imemuagiza, Kamishna na Maofisa wa Ardhi mkoani humo, kuhakikisha kila mwanaume anayefika kwenye ofisi za ardhi kuchukua hati ya kiwanja au shamba, aambatane na mke wake, na hati hiyo lazima iwe na jina la mwenza wake, ili kuondoa migogoro ya wanawake kudhulumiwa ardhi pindi mume anapofariki.
.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Martine Shigella, katika siku ya wanawake duniani ,huku akibainisha kuwa ,lengo ni kuwalinda wanawake dhidi ya dhuluma ya ardhi.