Serikali imesema asali inayozalishwa hapa nchini imekidhi viwango vya soko la kimataifa kwa asilimia 90 hivyo kuwa na soko kubwa kwa nchi za umoja wa ulaya ikiwemo ujerumani inayonunua asali nyingi kutoka hapa nchini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Mary Massanja ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti Maalumu Mh Jacqueline Kainja Mbunge wa viti maalimu CCM aliyetaka kujua serikali ina mpango gani kuhakikisha zao la asali inayozalishwa hapa nchini inapana soko la uhakika kimataifa.
Mh Massanja amesema kwa sasa asali ya Tanzania imeendelea kupata soko ulaya na mipango iliyopo ni kufufua na kuendeleza kwa nguvu uzalishaji kupitia mfumo wa mnyororo wa thamani ya ufugaji nyuki kwa mwaka 2021//2022 ambao unatarajiwa kuanzishwa mwaka huu.
Kadhalika Wizara ya maliasili na utalii imepanga kuanzisha viwanda vitano vha kuchakata mazao ya asali hapa nchini mpango utakaosaidia zaidi kuongeza thamani ya mazao ya nyuki kwa masoko ya umoja ya ulaya ikiwemo nchini ya Ujerumani ambayo ni wanunuzi wakubwa wa asali ya Tanzania kwa sasa.