Idara ya madini kanda ya kati Magharibi imetoa onyo kwa wachenjuaji wa madini ya Dhahabu katika eneo la Mwakitolyo wilayani Shinyanga wanaokwepa kulipa kodi ya serikali kwa kuvunja lakiri kenye maeneo yenye mchanga wa madini ya dhahabu uliozuiliwa na kutorosha mchanga huo hali ambayo imetajwa kuwa imeisababishia serikali kupata hasara kwa kukosa mapato.
Kaimu kamishna wa madini kanda ya kati Magharibi Joseph Kumburu ametoa onyo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kukagua maeneo ya wachenjuaji wa madini ya dhahabu waliofungiwa na serikali na kuelekezwa kurekebisha mifumi ya kulipa kodi ya serikali na kubaini baadhi ya lakiri zilizovunjwa na mchanga wenye madini kutoroshwa.
Baadhi ya wamiliki wa maeneo yaliyobainika kuvunjwa lakiri na mchanga kutoroshwa wakajieleza kwa kujitetea mbele ya kamishna wa madini na kuahidi kufuata sheria.
Na kisha kamishna wa madini Joseph Kumburu akalazimika kuitisha kikao cha dharura cha viongozi wa wachimbaji wadogo na wachenjuaji na kutoa agizo.