Jeshi la polisi mkoani Ruvuma limelazimika kufukua shimo katika kijiji cha Peramiho A na kuutoa mwili wa mtoto wa miaka sita Paul Haule, anayedaiwa kuuawa kwa kunyongwa na baba yake wa kambo Bwana. Richard Mgina na kufukiwa katika shimo hilo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Marco Chilya, amesema mtuhumiwa Mgina alimuua mtoto huyo kwa kumnyonga baada ya kukubaliana na Mkewe Ester Kayombo kwa imani za kishirikina ili watajirike.
ACP Chilya ameongeza kuwa wawili hao wanashikiliwa na polisi kwa kutekeleza mauaji hayo na watafikishwa mahakamani uchunguzi utapokamilika na kamanda huyo kuonya utajiri haupatikani kwa njia hiyo bali kwa kufanya kazi.
Diwani wa kata ya Peramiho Mhe.Nicholaus Lutengano na wananchi wa Kijiji cha Peramiho, wamelaani tukio hilo la kusikitisha dhidi ya mtoto huyo ambaye alikuwa akisoma elimu ya awali katika shule ya msingi Kilimani.