Back to top

BABA MBARONI KWA KULAWITI KICHANGA.

03 September 2024
Share

Mtoto mchanga wa miezi sita aliyefariki dunia, baada ya kudaiwa kulawitiwa na baba yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Damas Stephano, mwili wake unatarajiwa kuzikwa leo Septemba 03, 2024 katika makaburi ya Hijra ,mtaa wa Area A, jijini Dodoma.

Taarifa zinaeleza kuwa, baba mzazi wa mtoto huyo  baada ya kutekeleza jambo hilo, alikwenda kumtelekeza kwa bibi yake, kabla ya kupelekwa hospitali na kubainika kashafariki dunia.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Stella Mlewa amesema baba huyo  aliondoka na mtoto majira ya saa mbili usiku, na hakuwa na hofu kwa kuwa ni baba yake, lakini alianza kupata hofu, baada ya kuchukua muda mrefu bila kurudi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi George Katabazi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa tayari wanamshikilia mtuhumiwa huyo kwa uchunguzi zaidi.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania