Bodi ya Nyama Tanzania imepiga marufuku uuzaji wa nyama kwa mafungu katika maeneo ya nje ya machinjio ya vingunguti kwani inahatarisha afya ya mlaji.
.
Hayo yamesemwa na Kaimu Msajili wa bodi ya Nyama Tanzania Bw.Imani Sichalwe alipofanya ziara katika maeneo ya nje ya machinjio ya vingunguti na kusema uuzaji wa nyama kwa mafungu kiholela haukubaliki kwa mujibu wa Sheria na unaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa Kama kipindupindu na magonjwa Mengine ya matumbo kwa kuwa maeneo hayo ni machafu kuna mifereji ya maji taka kutoka katika vyoo na ni Maeneo ya wazi ambapo Kuna vumbi na kuhatarisha usalama wa nyama.
Bw.Imani Sichalwe amewataka wauzaji wa Nyama hizo kwenda katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya biashara hiyo lakini sio Maeneo Kama yale ya wazi.
.
"Hapa tunaona kinyesi na mikojo karibu na mnapouzia Nyama kwani ninyi hamuoni Kama ni hatari kwa afya,mlipuko kwa magonjwa ukitokea wa kwanza ni ninyi ambao hamfuati utaratibu hapa."Amesema Sichalwe.
.
Hata hivyo amesema kuwa dhumuni la serikali sio kuwakataza watu kufanya biashara bali kuwashawishi wafanyabiashara kufanya biashara zao katika hali nzuri na kuzingatia afya kwa mlaji.