Back to top

BUNGE LASITISHWA VINASA SAUTI VIMEPATA HITILAFU

31 October 2023
Share

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesitisha shughuli za Bunge, baada ya kutokea kwa hitilafu katika mfumo wa sauti.
.
Hali hiyo imejitokeza baada ya vinasa sauti na vipaza sauti katika Jengo la Bunge kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha ambapo sauti ilikuwa ikikatikatika.
.
Hata hivyo mafundi wanaendelea na matengenezo ya mfumo huo, huku shughuli za Bunge zikitarajiwa kuendelea baada ya nusu saa.