Mkuu wilaya ya Songwe Bw.Simon Simalenga ametishia kusitisha vibali vya shughuli za minada, magulio na masoko kwa muda usiojulikana iwapo wananchi wataendelea kupuuza maelekezo ya kujihadhari na janga la Covid-19 na kwamba suala la uvaaji barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka na kuepuka misongamano ni la lazima kutekelezwa.
.
Bw. Simalenga amesema halidhishwi na mwenendo wa wananchi katika kuzingatia taratibu zilizowekwa na serikali katika kukabiliana na virusi vya corona kwenye maeneo ya mikusanyiko, misongamano, mikutano na misiba.
.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema, kutokana na hali hiyo baadhi ya vibali havitatolewa kuanzia juma lijalo mpaka serikali itakapojiridhisha kuwa hali ya tahadhali hizo imeimarika.