Mkuu wa wilaya ya Songwe Simon Simalenga ,amewaagiza watendaji wa vijiji na kata katika tarafa ya Kwimba, kuwachukulia hatua kali baadhi ya wazazi kutoka jamii za wafugaji, wakulima na wavuvi, ambao wanadaiwa kuwashawishi wanafunzi wanaotakiwa kuanza darasa la kwanza na kidato cha kwanza kutoripoti shuleni, na badala yake kuwatumia katika shughuli zao, hali inayosababisha zoezi la kuripoti kwa wanafunzi hao kusuasua.
Dc Simalenga ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na walimu wakuu, watendaji wa vijiji na kata kutoka tarafa hiyo .