Mkuu wa wilaya ya Songwe Simon Simalenga amewasimamisha kazi viongozi wote wa kijiji cha Saza ili kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za wizi wa makinikia ya dhahabu, utawala wa mabavu na kuminya uhuru wa wananchi kujieleza, malalamiko yaliyoibuliwa na wananchi kupitia vituo vya ITV/Radio One.
Simalenga ataitisha mkutano wa hadhara tarehe 4 Julai ili kuweka bayana matokeo ya uchunguzi Huo baada ya kuthibitisha uhalali wa tuhuma hizo.