Back to top

DIT yaanza mfumo wa kuunganisha magari kwenye gesi.

12 June 2019
Share

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imeanza kuunganisha magari  kwenye wa mfumo wa matumizi  ya gesi asilia badala ya petroli na kwamba mpaka sasa zaidi ya magari 150 yameshaunganishwa katika mfumo huo.

Akizungumza na ITV Digital Mratibu wa Gesi Asilia kwenye Magari kutoka DIT, Dkt.Esebi Nyari amesema mfumo huo wa kuunganisha gesi asilia badala ya mafuta ya petroli unasaidia kupunguza gharama kwa wamiliki wa magari na kiasi kidogo cha gesi kinakuwa kinatumika.

Dkt.Esebi Nyari amefafanua kwamba wanachokifanya sasa hawaondoi mfumo wa gari uliopo bali wanaongeza mfumo mwingine, ambapo kutakuwa na mfumo wa Petroli na Gesi, hivyo mmiliki wa gari anaweza kutumia njia zote mbili akiishiwa Petroli ana tumia Gesi.

Amesema Gesi ambayo wanaifunga kwenye gari haina madhara na hailipuki, kwani wengi wanadhani kwamba labda nikama gesi ya kupikia, jambo ambalo amewatoa wasiwasi wamiliki wa magari na kusema ipo salama na nigesi ambayo haichafui mazingira.

Kwa sasa amesema sehembu ya kujazia Gesi hiyo ni DIT au Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam na mfumo huo watu wakizidi kuupenda wataongeza vituo vya kujazia gesi hiyo.

Dkt.Nyari ameongeza kwa kusema kuwa mfumo huo faida zake ni kubwa mnoo kwani gesi asilia kilo  moja 1,450, huku petroli lita moja ikigharimu kiasi cha shilingi 2,200 lakini ukitumia gesi asilia unatembea na gari umbali mrefu, ambapo kilo moja ya gesi asili ni kilometa 20, Petrol litamoja inakwenda kilometa 12.  

Mratibu wa Gesi Asilia kwenye Magari kutoka DIT, Dkt.Esebi Nyari akionesha namna gari hii inavyotumia gesi, huku akisema Gesi ambayo wanaifunga kwenye gari haina madhara na hailipuki kama wengi wanavyodhani, huku akiwatoa hofu watumiaji kwamba gesi hiyo sio kama ile ya kupikia majumbani.