Back to top

FCT YACHOCHEA UWAJIBIKAJI ,UBUNIFU, KUSIMAMIA HAKI

21 April 2024
Share

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Bw.Abbas Rugwa, amesema kusikilizwa na kufanyiwa kazi kwa asilimia 97 ya mashauri yaliyowasilishwa kwenye Baraza la Ushindani nchini (FCT) ,kumechochea na kuongeza uwajibikaji kwa Mamlaka za Udhibiti wa Huduma na Biashara nchini ,katika kusimamia ushindani wa haki. 

Amesema Serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha inaweka mazingira rafiki na wezeshi ya ushindani wa haki katika biashara na utoaji huduma , na kuzitaka mamlaka za udhibiti kutekeleza azma hiyo ya serikali.

Amesema tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo mwaka 2007 hadi sasa, jumla ya mashauri 442 yamewasilishwa mbele ya baraza hilo, ambapo kati yake mashauri 429 sawa na asilimia 97 yamesikilizwa na kutolewa maamuzi.