Back to top

GARI LA MASHINDANO LAUA 7, LAJERUHI 21 SRI LANKA.

22 April 2024
Share

Watu saba wamefariki na wengine 21 kujeruhiwa ,baada ya gari la mashindano kuwaparamia watazamaji katika mashindano ya magari Fox Hill Supercross, siku ya Jumapili huko Diyatalawa, nchini Sri Lanka.

Miongoni mwa waliofariki ni maafisa wanne wa mashindano hayo,  na watazamaji, akiwemo msichana wa miaka minane.

Mamlaka zimesema uchunguzi kamili wa polisi unaendelea kuhusu tukio hilo ,ambapo Msemaji wa Polisi Nihal Talduwa amesema "ajali hiyo ilitokea pale gari lilipopoteza uelekeo na kuhama njia.

Kwa mujibu wa mashuhuda, wamesema ajali hiyo ilitokea mara baada ya gari lingine kupinduka kwenye njia, huku baadhi ya raia wa Sri Lanka wakikosoa ukosefu wa vizuizi vya usalama kwenye safu kadhaa za njia.