Back to top

Halmashauri ya wilaya Songea yashindwa kushiriki maonesho ya nanenane

05 August 2018
Share

Katika hali isiyokua ya kawaida halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imeshindwa kuandaa Banda la maonesho ya siku ya wakulima mkoani Ruvuma hatua ambayo mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw. Pololeti Kamando Mgema amekemea udhaifu huo na kwamba unawanyima haki ya msingi wakulima kujifunza kilimo bora ili kwenda kwenye uchumi wa kati.
 
Katika maoenesho ya nane nane mwaka huu mkoani Ruvuma, mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw.Pololet Kamando Mgema ameshuhudia milango ya banda la halmashauri ya wilaya ya Songea ikiwa imepigwa kufuli, hali ambayo ameuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kujitathimini upya kwa kuwanyima haki ya msingi wakulima kupata elimu ya kilimo bora na kwenda kwenye uchumi wa kati.
 
Aidha, katika banda la halmashauri ya wilaya ya Mbinga, Bw. Mgema akakutana na changamoto ya vijana wanaotengeneza bidhaa za ngozi kukosa mikopo licha ya kuomba mara kadhaa kwenye halmashauri hiyo, hatua ambayo pia akalazimika kutoa maagizo.
 
Hata hivyo baadhi ya wadau wa maendeleo mkoani humo, wamesema licha ya mkoa wa Ruvuma kuwa wa nne katika uzalishaji wa mazao ya chakula hapa nchini lakini inaongoza kwa kuwa na watoto wengi wenye ugonjwa wa utapiamlo.