Picha hii kwa hisani ya Mtandao.
Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo mkoani Dodoma imekuwa hospitali ya pili nchini kuweza kufanya upandikizaji wa figo baada ya ile ya taifa ya muhimbili ya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo kaimu Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Dkt. Alphonce chandika amesema upandikizaji huo wa figo ulifanywa kwa ushirikiano kati ya madaktari wa hapo na wale wa kutoka nchini JAPAN.
Katika hatua nyingine balozi wa Kuwait nchini Jaseem al Najeem amesema nchi yake ipo katika mchakato wa kuangalia mapungufu yaliyopo katika hospitali hiyo ili iweze kuisaidia na kuifanya iwe ya kisasa zaidi.
Balozi Al Najeem amesema hayo wakati akikabidhi msaada uliotoka nchini humo na kupitia taasisi ya doris foundation kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.