Idadi kubwa ya viwanda vidogo vya kuchakata vyakula matunda ngozi na mafuta ya kula hapa nchini vimedorora kutokana na kukosa mitaji kunakodaiwa kusababishwa na ukosefu wa mipango mizuri ya uendeshaji biashara.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuendeleza viwanda vidogo SIDO Prof Silvester Mpanduji ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wadau wa viwanda vidogo pamoja na watalam wa biashara na mikopo kutoka SIDO wanaokutana jiji Arusha.
Meneja wa Mikopo kutoka SIDO Makao Makuu Haika Shayo anasema kinachoangusha wafanyabiashara wadogo ni kukosa utaalam wa kuandaa maandiko yatakayokubalika kwenye taasisi za fedha.