Back to top

Jaji Mkuu wa Tanzania aagiza kupelekewa mashauri ya kesi za miradhi.

23 February 2019
Share

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Juma ameagiza kupelekewa orodha za mashauri ya kesi za mirathi ambazo hazijakamilika ndani ya muda wa kisheria uliowekwa ili kutafuta mkakati maalum wa kuzishughulikia ambazo kwa sasa zimeonyesha kuwa ni kero.

Jaji mkuu Prof.Juma ametoa agizo hilo wakati akiwaapisha mahakimu wakazi wa mahakama za mwazo daraja la pili na kusema ucheleweshaji wa kesi hizo umepelekea wasimamizi wa mirathi kijinufaisha.

Hata hivyo baadhi ya mahakimu walioapishwa wanasema watatumia nafasi hiyo kufanya kazi ya umma kwa kusimamia sheria haki na wajibu.

Mahakimu hao pia wameaswa kufanya kazi kwa weledi ili mahakama iendelee kuwa kimbilio la kutafuta haki kwa wananchi wa ngazi zote.