
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Jacob Mkunda amelitaka jeshi la Tanzania kamandi ya wanamaji kuendelea na umuhimu wa kufanya mazoezi ya utayari kwa lengo kujihami na kujipima uwezo katika kutathimini mbinu na mikakati ya jeshi hilo.
Ameeleza hayo wakati wa kufunga mazoezi hayo ya utayari yaliyofanyika Kisiwa cha Mziha, Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Mazoezi hayo yanayojulikana kama Papa Potwe 2023, yameanza kufanyika tarehe 12 mwezi Juni mwaka huu katika kisiwa hicho kilichopo bahari ya hindi.