Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshma lililoandaliwa na vikosi vya Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma kwa ajili ya kuhutubia pamoja na kulifungua rasmi Bunge hilo la 12 leo tarehe 13 Novemba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia pamoja na kulifungua rasmi Bunge hilo la 12 leo tarehe 13 Novemba 2020 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kufungua Bunge la 12 leo tarehe 13 Novemba 2020 jijini Dodoma, Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi.