Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 01 Aprili, 2021 atamuapisha Katibu Mkuu Kiongozi na atawaapisha Mawaziri 8 na Naibu Mawaziri 8 ambao aliwateua jana baada ya kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri.
Uapisho huo utafanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma kuanzia saa 9:00 alasiri.
Katibu Mkuu Kiongozi atakayeapishwa ni Mhe. Balozi Hussein Athuman Katanga.
Mawaziri Wateule watakaoapishwa ni Mhe. Ummy Ally Mwalimu (kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI), Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (kuwa Waziri wa Katiba na Sheria), Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (kuwa Waziri wa Fedha na Mipango) na Mhe. Selemani Saidi Jafo (kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira).
Mawaziri Wateule wengine watakaoapishwa ni Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo (kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara), Mhe. Geoffrey Idelphonce Mwambe (kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji), Mhe. Balozi Liberata Rutageruka Mulamula (kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki) na Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).
Naibu Mawaziri Wateule watakaoapishwa ni Mhe. William Tate Ole Nasha (kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji), Mhe. Abdallah Hamis Ulega (kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi), Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara (kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi) na Mhe. Pauline Philipo Gekul (kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo).
Naibu Mawaziri Wateule wengine watakaoapishwa ni Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango), Mhe. Mbarouk Nassoro Mbarouk (kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki), Mhe. Mwanaidi Ally Hamis (kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) na Mhe. Hamad Hassan Chande (kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira).