
Kiongozi wa Azimio la Umoja One Kenya, Bi.Martha Karua, amewataka wakenya kutoka majumbani kwao na kujiunga na maandamano, kesho Jumatano, Julai 19, 2023, wakiwa na masufuria kuashiria ukosefu wa chakula ambao amedai umesababishwa na gharama ya juu ya maisha.
.
Aidha, Bi. Karua amewataka wote waliorekodi picha zilizonasa unyanyasaji wa aina yoyote ya ukatili wa polisi kwenye maandamano yaliyofanyika wiki jana, kuziwasilisha, kwa ajili ya kuzifikisha mahakamani.