
Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia watu 3 wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kujifanya maafisa kutoka Ikulu wakituhumiwa kuwatapeli Wakurugenzi wa Halmashari, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Taasisi za serikali wakiwadanganya kuwa Mhe.Rais ameridhishwa na utendaji kazi zao hivyo wanapaswa kutuma pesa ili kupata nafasi za juu zaidi serikalini.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Henry Mwaibambe amethibitisha, huku akieleza kwamba watuhumiwa hao wamekamatwa na idadi kubwa ya simu za mkononi na laini nyingi za simu zikiwa na majina ya viongozi wakubwa waandamizi wa serikalini.