Back to top

Maalim Seif rasmi sasa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

08 December 2020
Share

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Mheshimiwa Maalim Seif Sharrif Hamad ameapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kuridhia kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais Dakta Hussein Ali Mwinyi.

Sherehe za kuapishwa kwa Maalim Seif zilizofanyika ikulu ya Zanzibar, zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vinavyounda serikali hiyo akiwemo Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Mhe.Zitto Kabwe.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Mhe.Maalim Seif amesisitiza umuhimu wa maridhiano katika kujenga umoja wa kitaifa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi wenzake kuijenga Zanzibar.

Kwa upande wake, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameahidi kutimiza wajibu wake  kusisitiza umuhimu ushirikiano kati ya serikali ma wananchi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi