Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesema idadi kubwa ya waliojitokeza kupima maambukizi ya virusi vya UKIMWI baada ya kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha utambuzi wa afya, matokeo chanya yanatokana na wanaume, huku maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI nchini yamepungua kutoka asilimia 7 hadi 4.
Waziri Mkuu, ameyasema hayo katika hotuba yake katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Amesema serikali imefanikiwa kufikia malengo ya milenia ya 90 tatu katika kukabilina na vurusi vya UKIMWI hapa nchini na kwamba tatizo kubwa kwa sasa ni ongezeko la maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 24.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Bwana Leonard Maboko amesema kwa sasa jitihada zinaendelea kukabilina na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa vijana.
Mwakilishi mkazi wa umoja wa mataifa aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Zlatan Millisic amesema wataendelea kushirikiana na Tanzania kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI ili kufikia malengo ya kupunguza makali na kufubaza virusi kipitia mpango wa tisini tatu ifikapo mwaka 2030 .
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni 'Mshikamano wa Kimataifa, Tuwajibike Pamoja.