Back to top

Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yapungua Tanga.

29 May 2022
Share

Halmashauri ya Jiji la Tanga imepongezwa kwa kupunguza  kiwango cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka 3.5%  mwaka 2020 hadi kufikia 3.2% kwa mwaka 2021.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu  Mhe. Ummy Nderiananga alipokuwa akipokea taarifa ya Mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI ya Mkoa wa Tanga ambapo pia alibainisha kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kupitia bajeti mpya ya serikali 2022-2023 itakayoanza mwezi wa saba ameongeza fedha kwenye eneo hilo.