![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/mabasi%20mwanza.jpg?itok=tOqvam69)
Wamiliki wa mabasi yaendayo mkoani zaidi ya mia moja jijini Mwanza wagoma kubeba abiria katika stendi kuu ya mabasi ya Nyegezi huku wakidaiwa kupinga mfumo mpya wa ukataji wa tiketi kwa njia ya kielektoniki na kusababisha adha kwa abiria.
.
Akizungumza katika stendi hiyo ya mabasi Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) mkoa wa Mwanza Halima Lutavi amekiri kuwepo kwa mgomo huo.