Back to top

Mabasi yanayosafirisha abiria kati ya Mbeya na Mwanza yameanza mgomo.

10 March 2021
Share

Abiria waliokuwa wakitarajia kusafiri kutokea jijini Mbeya kuelekea mikoa ya kanda ya ziwa leo wamekwama katika Kituo Kikuu cha Mabasi jijini Mbeya baada ya mabasi yote yanayosafirisha abiria kati ya Mbeya na Mwanza kuanza mgomo uliotangazwa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Nchini(TABOA)  wakipinga matumizi ya tiketi za kimtandao.
.
Alfajiri ya siku ya leo mabasi yanayosafirisha abiria kuanzia katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha jijini Mbeya kuelekea maeneo mengine kama vile Dar es salaam, Arusha, Dodoma na Songea yameondoka kama kawaida, isipokuwa yale yanayoelekea kanda ya ziwa ambayo hajasafiri na ndipo mawakala wa mabasi hayo wakaeleza sababu za kusitisha safari zao.
.
Afisa mfawidhi wa Mamlaka Ya Udhibiti Wa Usafiri Wa Nchi Kavu, (LATRA) Kanda ya Nyanda za juu kusini, Denis Daud anathibitisha kuwepo kwa mgomo huo  na hatua zinazochukuliwa na ofisi yake kukabiliana na changamoto hiyo.