Back to top

Maduka ya pembejeo za kilimo yafungwa Mtwara

22 June 2019
Share

Zaidi ya maduka kumi na tano ya pembejeo za kilimo yamefungwa katika wilaya za Newala na Masasi mkoani Mtwara baada ya kukiuka taratibu za afya ikiwemo kuchanganya sumu za kuua wadudu waharibifu pamoja na vyakula na wengine wakizianika juani huku zikitoa harufu kali  hali inayotajwa kuweza kusababisha magonjwa ya saratani kwa wauzaji na watu wanaokula vyakula hivyo

Katika operesheni iliyofanywa na watafiti wa visumbufu mazao na mimea, maduka hayo yaliyokutwa yakiuza sumu hizo karibu na vyakula kama samaki maharage na vingine huku harufu kali ya sumu hizo ikiwa imeenea katika eneo hilo  wataalam wanadai inaweza kusababisha magonjwa kama kansa na mengineyo na hata hivyo ni kinyume na sheria ya afya ya mimea ya mwaka 1997.

Baadhi ya watu waliyokutwa na makosa wakakiri kufanya hivyo bila kujuwa na kuomba wasamehewe ili waweze kufuata utaratibu.

Wauza pembejeo wanaofuata taratibu wanasema wamekuwa na wakati mgumu unaotokana kukithiri kwa uuzwaji holela wa sumu hizo wameshukuru wakaguzi kufanya operesheni hiyo.