Teknolojia mpya ya magari yanayotumia umeme imetambulishwa rasmi ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo aina hiyo ya teknolojia inatajwa kuwa ya kwanza na ya aina yake kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
Wadau walio kwenye sekta ya utalii wanasema kutokana na desturi ya wanyama kutokupenda kelele , magari hayo ya kutumia umeme yatafaa zaidi kutokana na kutokua na muungurumo lakini pia wakieleza kuwa ni teknolojia rafiki kwa mazingira..