
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imepokea kesi ya kupinga uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyofunguliwa na Ally Saleh 'Alberto' ambaye alikuwa moja ya wagombea kwenye uchaguzi huo.
Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika tarehe 8 Agosti, 2021, jijini Tanga, ambapo mpaka sasa kamati ya uchaguzi imempitisha Wallace Karia kuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya Urais.
Kesi hiyo ya madai namba 98 ya mwaka 2021, iliyofunguliwa na Ally Salehe, raia wa Tanzania anayeishi Zanzibar ambayo itakuwa chini ya Jaji Kakolaki ambapo wadai ni TFF, Bodi ya wadhamini na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Kiomoni Kibamba.
Mahakama hiyo pia imewataka wadaiwa hao wote watatu kufika kesho mahakamani hapo, kujibu hoja ya kwanini uchaguzi huo usisimamishwe.