Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko wamewatakiwa wanachama wao heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.
Wawili hao wametoa heri hiyo katika Mahakama y a Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi yao ya uchochezi inayowakabili na viongozi wengine saba wa chama hicho.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa.
Wakili Simon amedai kuwa hawana taarifa ya kinachoendelea mahakama ya juu hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hata hivyo, Wakili Faraja Mangula alidai kuwa Wakili wa washitakiwa hao Peter Kibatala na Sheck Mfinanga wamepata dharura hivyo wanaomba mahakama ipange January 4, mwakani.