Back to top

Mahakama ya Kisutu yawapiga stop Mashinji na Matiko kusafiri.

25 September 2019
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewakatalia ombi la kusafiri nje ya nchi viongozi wa CHADEMA, Vincent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini Mhe.Esther Matiko wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi na kusisitiza viongozi hao kuwaaanda mashahidi haraka ili kuendelea na kesi inayowakabili.

Uamuzi huo umetolewa leo, Septemba 25, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.

Hakimu Simba amesema endapo atawaruhusu washtakiwa hao wasafiri nje ya nchi, kesi hiyo itashindwa kuisha kwa wakati.